Polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya imefanikiwa kuteketeza mashamba makubwa ya bangi pamoja na nyumba zinazotumiwa kama sehemu ya maficho na wakulima wa zao hilo haramu huku ikifanikiwa kukamata zana mbalimbali za kilimo zilizokuwa zikitumiwa na wakulima wa bangi huko katika kijiji cha Wegita wilayani Tarime mkoani Mara.
Msako mkali unaoendeshwa na kamati ya ulinzi na usalama wilayani Tarime unabaini nyumba zilizotumika kama maficho ya wahalifu hao pamoja na mashamba makubwa ya bangi katika kijiji cha Wegita.
Zoezi la kufyeka na kuteketeza mashamba pamoja na nyumba za wahalifu likaanza mara moja chini ya mwenyekiti wa kamati hiyo Bw. GLORIUOS LUOGA.
Baada ya kukamilika zoezi kuteketeza nyumba pamoja na zao haramu la bangi sasa ikawa ni zamu ya viongozi kuelezea azma ya oparesheni hiyo na hapa mkuu wa polisi wilaya ya kipolisi ya Tarime BW. THOMAS MAPULI anafafanua.
Na kisha Serikali ikaeleza ilivyofanikiwa kuendeleza mapambano dhidi ya wakulima wa zao hilo.