Rais mpya wa Gambia Adama Barrow, ameondoka nchini Senegal akielekea nchini mwake kuchukua hatamu uongozi.
Barrow aliapishwa wiki iliyopita Senegal wakati viongozi wa kieneo walipokuwa wakimshawishi kiongozi aliyekuwepo ajiuzulu.
Wanadiplomasia wamemtaka Barrow arudi mara moja nyumbani kuepuka pengo la uongozi.
Taarifa zinasema Barrow atakaa katika makaazi yake wakati ukaguzi ukifanywa katika ikulu kutambua hatari yoyote kufuatia kuondoka kwa Yahya Jammeh kwenda uhamishoni Guinea ya Ikweta.
Maelfu kadhaa ya wanajeshi wa mataifa ya Afrika magharibi wanasalia Gambia wakati kukiwa na taarifa kuwa wafuasi waovu wa Jammeh wamo miongoni mwa vikosi vya usalama nchini.