SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 26 Januari 2017

T media news

Mahakama ya wilaya Kahama Mkoani Shinyanga hii leo imewahukumu watu wawili kwenda jela mwaka mmoja


Mahakama ya wilaya  Kahama Mkoani Shinyanga hii leo imewahukumu watu wawili  kwenda jela mwaka mmoja au kutoa faini  ya Tsh laki mbili kila mmoja kwa kosa la kuingia katika pori la  kigosi lilopo wilayani humo bila kibali cha mkurugenzi wa maliasiliri.

Hukumu hiyo imetolewa na hakimu mkazi wa mahakama hiyo Mhe,Kenethi Mtembei baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ambapo watuhumiwa hao walikili kutenda kosa hilo ambao ni Manyanda Charles mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa kijiji cha Nyankende na Yela  Mwenelwa mwenye umri wa miaka 40 mkazi wa Nsango.

Awali mwendesha mashitaka wa NyamaPoli Catherin Aloys amesema washitakiwa walitiwa hatiana kwa kukiuka kifungu cha sheria namba 15 (1) (2)  namba  5 ya mwaka 2009 na walikamatwa January 21 mwaka huu majira ya tano asbuh maeneo ya Migu lilopo  ndani ya hifadhi Kigosi na kufikishwa Mahakamani January 22 Mwaka huu  na kukili kutenda kosa hilo.

Kabla ya hukumu kutolewa mshtakiwa namba mbili ambaye ni Yela Mwenehlwa ambaye aliomba mahakama imsamehee kwa kuwa amekili kutenda kosa hilo huku mwendesha mashitaka akiomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo.