SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 7 Novemba 2016

T media news

TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA KIMATAIFA WA BIASHARA


Na Amina Kibwana, Globu ya Jamii 

TANZANIA  kufikia  uchumi wa viwanda  mwaka 2020  kunahitajika kuwa na mazingira yatakayoweza kuwavutia wawekezaji  watakaoweza kuwekeza viwanda ikiwa ni pamoja na kuimarisha viwanda vidogo  vidogo katika kuzalisha bidhaa kwa wingi 

Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar,Mkurugenzi Mtendaji wa  Mfuko wa Sekta Binafsi Nchini (TPSF),Godfrey Simbeye ameyasema hayo wakati  akitangaza mkutano wa Kimataifa  uunaotarajiwa kufanyika Desemba 5 hadi 7 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere  jijini Dar es Salaam.

Simbeye amesema kuwa mkutano  huo utazishirikisha nchi mbalimbali Duniani ambazo zimepiga hatua  katika sekta ya viwanda,ambapo wawekezaji watapata fursa za kuwekeza katika sekta ya  viwanda nchini.

Mkutano huo ambao umeandaliwa na TPSF kwa kushiriana na  tasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo Wizara ya Viwanda,Biashara, Arusha ya International Conference Centre, Shirika la Viwanda Vidogo, Vido IDO,TIC,EPZA,ZIPA,TTB pamoja na TANTRADE ambapo kwa pamoja wataingaza Tanzania katika  sekta ya viwanda nchini ili iweze kuleta matunda kwa watanzania pamoja kukuza uchumi.

Simbeye amesema mkutano kama huo  ulishafanyika mara mbili  katika nchi za Afrika ikiwepo  Misri na Afrika Kusini  na Tanzania imepata nafasi ya tatu katika kufanyika mkutano huo  ambapo ni fursa ya Tanzania katika  kuelekea uchumi wa viwanda kufikia 2020.

Amesema kampuni ya Biashara  nchini yatafaidika katika kutanua  uwigo wa mitandao ya kibiashara na kubadilishana uzoefu, taaluma  za kuweza kufanya fursa za uwekezaji, kuonyesha uwepo wa nchi katika jukwaa la kimataifa pamoja na kuongeza ushawishi na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kutokana na kuongezeka mzunguko wa fedha za kigeni nchini  kutokana na ujio wa wageni wataoshiriki mkutano huo.

"Tanzania tunajivunia kuwa nchi ya tatu katika kufanyika mkutano huu, hii ni fahari sana kwetu, kwani tunaanza kuonekana kuwa nchi yetu ina hadhi” amesema Simbeye.

Sembeye  amesema mikutano kama hii inapokuja katika Nchi yetu inawapa watu fursa ya kuhudhuria na kufaidika pia inasaidia kukuza uchumi kwani tunategeme kupata wageni  400 ambapo wageni 200 watatoka nje ya nchi."  

Aidha ameongeza kuwa mkutano huo utakuwa sambamba na maonesho ya viwanda  yatakayoanza Desemba 7 hadi 11 mwaka huu ambapo washiriki wa mkutano watapata fursa ya kutembelea maonesho hayo. Simbeye amesema Tanzania ina jumla ya viwanda 49000, lakini viwanda vikubwa vipo 2000 tu hivyo hii ni fursa kwetu kutangaza bidhaa zetu.