SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 4 Novemba 2016

T media news

Paul Makonda Kupanda Kizimbani Jumatatu


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  Jumatano ijayo anatarajiwa kupanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujitetea dhidi ya kesi ya madai ya Sh200 milioni iliyofunguliwa na waliokuwa makada wa CCM, Mgana Msindai na John Guninita.

Makonda anayetetewa na Wakili wa kujitegemea Seneni Mponda, atatoa utetezi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba.

Msindai na Guninita wanatetewa na mawakili kutoka Kampuni ya Uwakili ya BM; Benjamin Mwakagamba na Ester Shedrack.

Katika kesi hiyo ya madai namba 68 ya 2015, Msindai na Guninita wanaiomba Mahakama kumuamuru Makonda awaombe msamaha na kumlipa kila mmoja Sh100 milioni.