Mamlaka ya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA
upo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wa upanuzi wa uwanja huo utakaowezesha kupokea zaidi ya abiria milioni moja kwa mwaka pamoja na kutua ndege kubwa kumi na moja kwa wakati mmoja mradi unaenda pamoja na ufungaji wa vifaa vya kisasa vya ukaguzi hili kudhibiti uharifu.
Akizungumza na ITV Meneja wa Mradi wa upanuzi wa uwanja huo Mhandisi Mathew Ndossi amesema utakapo kamilika siku chache zijazo uwanja wa KIA utakuwa mi miongoni mwa viwanja vyenye uwezo mkubwa wa kupokea abiria wengi na ndege nyingi kubwa hali itakayo fanikisha wanja huo kuingiza fedha nyingi za kigeni.
Mkurugenzi wa uendeshaji na ufundi wa kampuni ya usimamizi wa uwanja huo KADCO Christopher Mukoma amesema baadhi ya mashine za ukaguzi zimeshafungwa kwenye uwanja huo na matukio ya upitishaji wa dawa za kulevya na nyala zingine za serikali yamepungua kwa kiasi kikubwa.