MALAWI: Mwanaume Eric Aniva, aliyeshiriki ngono na wanawake tofauti 104 akitekeleza mila huku akijua ameathirika na UKIMWI, amehukumiwa kifungo cha miaka 2 jela.
Amepatikana na hatia ya kutekeleza mila zenye madhara chini ya sheria za jinai za taifa hilo
Wanawake wawili wajane waliotoa ushahidi mahakamani walisema walilazimishwa kufanya mapenzi na mtu huyo ili kutakasa roho za waume zao ambao walishafariki.