Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ametilia shaka juu ya ari ya kupambana kwa baadhi ya wachezaji wake, licha ya timu yake kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Swansea City. jana.
Mourinho alilazimika kutumia mabeki wasio wa asili kwenye mchezo huo, ambapo wachezaji wawili asilia kwenye nafasi hizo Chris Smalling and Luke Shaw waliondolewa kabla ya mchezo, wakati Daley Blind pekee ndiye beki aliyepata nafasi ya kubaki kwenye benchi.
Ashley Young, Phil Jones, Marcos Rojo na Matteo Darmian ndiyo waliongoza ukuta wa United, huku Mourinho akitoa kauli kuhusu wachezaji ambao walionekana kutokuwa fiti katika mchezo huo.
“Nina rafiki yangu ambaye ni mchezaji mkubwa sana wa tennis na huwa ananiambia wakati ambao hucheza akiwa na maumivu na wakati ambao kucheza bila maumivu.
“Ili kushindana ni lazima upambane mpaka ukomo wako. Hii ni tabia kwa baadhi ya watu, na huo si utamaduni wangu.Ni zaidi ya utamaduni wangu, ni utamaduni wa Manchester United.
“Tuna wachezaji wenye matatizo sana. Kwenye kila mchezo, na najua kwasababu nina marafiki wengi kwenye michezo tofauti na wanachezaji kwenye kiwango cha juu sana, na unajua mara ngapi wanacheza wakiwa hawapo fiti kwa asilimia 100!!”
United wanashika nafasi ya sita katika msimamo wa Premier League baada ya kucheza michezo 11, pointi nane nyuma ya vinara wa ligi hiyo Liverpool.