SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 23 Novemba 2016

T media news

Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) Yataadharisha Kuhusu Uwezekano wa Kuja Kwa Mvua Kubwa

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) yataadharisha kuhusu uwezekano wa kuja kwa mvua kubwa yenye upepo, yawataka wananchi wachukue tahadhari.

Yasema mabadiliko ya hali ya hewa kwa sasa yanatokana na kuwepo kwa msimu unaotawaliwa na uwepo wa LANINA ambayo ni ongezeko la hali ya baridi katika eneo la Ikweta ya Bahari ya Pasifiki.

Bado matarajio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa na upepo vitaendelea kuwepo katika msimu huu mpaka mwezi Disemba na mabadiliko kidogo yatajitokeza kwa baadhi ya mikoa ambapo mvua zitanyesha kwa wastani.