SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 6 Oktoba 2016

T media news

TRA YAKUSANYA TRILIONI 1.37 MWEZI SEPTEMBA

Mamlaka ya mapato nchini, TRA imekusanya shilingi trilioni 1.37 kwa mwezi Septemba, nyuma kidogo ya lengo la kukusanya trilioni 1.4 kwa mwezi huo.

Mkurugenzi wa elimu kwa mlipa kodi wa TRA, Richard Kayombo amesema mwenendo wa ulipaji wa mapato ya serikali ni wakuridhisha katika kufikia lengo la kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 15.1 kwa mwaka wa fedha 2016,2017.

“Katika mwezi wa tisa mamlaka ya mapato Tanzania imekusanya jumla ya shilingi za kitanzania trilioni 1.37 na mkiangalia katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka wa fedha 2016 2017 mpaka sasa hivi, kwa maana ya mwezi Julai mwezi Agosti na mwezi Septemba tumeshakusanya jumla ya shilingi trilioni 3.59. Nadhani tunaendelea vizuri,” alisema.

“Na tukumbuke kwamba makusanyo hayo ni sehemu ya lengo la mwaka 2016/2017 la trilioni 15.1,” alisema.

BY: EMMY MWAIPOPO