Kwa Ufupi, Taarifa Inasema:
=> Taarifa kuwa kuna upungufu mkubwa wa dawa katika Bohari Kuu ya Dawa si za kweli
=> Suala la Afya ni kipaumbele kwa Serikali ya Awamu ya Tano
=> Hali ya upatikanaji wa dawa kwa sasa iko vizuri. Zipo antibiotics muhimu kama Amoxycillin, Ciprofloxacin, Cotrimoxazole na Doxycycline.
=> Aidha, taarifa inabainisha kuwa dawa za maumivu kama Paracetamol, Asprin na Diclofenac zipo za kutosha.
=> Taarifa inaongeza kuwa kuna dawa za Kifua Kikuu, Ukoma na zile za kufubaza makali ya UKIMWI(ARVs) zipo.
=> Chanjo za watoto na wajawazito - kweli kulikuwa na uhaba miezi 2 iliyopita lakini sasa zipo.
=> Wiki iliyopita, serikali imenunua na kupokea dozi milioni 2 za chanjo ya Kifua Kikuu(BCG) na Dozi milioni 1.2 za Polio na zinasambazwa ktk vituo vya afya nchini.
=> Hakuna haja ya bajeti ya dharura kwa hili.
=> Zimeshatengwa Sh. Bilioni 85 kulipa deni la MSD lililokuwa likidaiwa.
=> MSD haitapatiwa mshindani, itakuwa ni kurudufisha (duplication) majukumu.