SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 8 Oktoba 2016

T media news

Rekodi za Argentina ikiw na Messi na bila Messi kufuzu Kombe la Dunia

Miamba ya soka la bara la Amerika ya Kusini timu ya taifa ya Argentina ililazimishwa sare ya pili mfululizo na Peru kwa kufungana magoli 2-2 ikiwa imetoka kupata matokeo kama hayo mwezi uliopita dhidi ya Venezuela.

Wakati Lionel Messi akiwa nje ya uwanja akiuguza majeraha, kocha wa Argentina Edgardo Bauza aliwaita washambuliaji wanne kwenye kikosi chake wakiongozwa na Angel Di Maria, Sergio Aguero, Paulo Dybala pamoja na Gonzalo Higuain.

\Licha ya kuwa na safu kali ya washambuliaji wenye vipaji, Argentina imeshindwa kutetea ushindi wake katika mechi mbili ambapo ililazimishwa sare licha ya kuwa mbele ya wapinzani wake kwa mabao. Kwa sasa inakamata nafasi ya tano kwenye kundi lake la kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018.

Argentina ikiwa na Messi na bila Messi

Nyota huyo wa Barcelona mwenye miaka 29 alishawishiwa kurejea kwenye timu ya taifa baada ya kutangaza kustaafu kufatia kuchapwa kwa mara ya pili mfululizo kwenye fainali ya Copa America na timu ya taifa ya Chile.

Rekodi ya Argentina ikiwa na Messi na ikiwa bila Messi inaonesha kuna tofauti kubwa kwasababu katika mechi 6 za Argentina bila Messi imeweza kupata ushindi kwenye mchezo mmoja pekee.