SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 8 Oktoba 2016

T media news

Hleb awatabiria Arsenal ‘treble’ msimu huu



Mchezaji wa zamani wa Arsenal Alexander Hleb anaamini kwamba kikosi cha sasa cha Arsene Wenger kina uwezo wa kubeba mataji matatu kwa mpigo msimu huu.

Arsenal wamekuwa na matokeo mazuri katika michezo ya hivi karibuni, wakiwa na alama mbili pungufu dhidi ya vinara wa EPL,vilevile wakiwa wamejikusanyia alama nne katika michezo miwili kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Na sasa, Hleb ambaye wakati yupo Arsenal hakuwahi kushinda taji lolote anaona ubora wa sasa wa Arsenal ni wa kuchukua mataji matatu msimu huu.

“Naamini Arsenal watashinda mataji matatu msimu hu, ubingwa wa Premier League, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa pia,”Hleb amesema. ” Naiona Arsenal yenye uwezo na ari ya kupambana na kwa hakika nitaisapoti.”

“Mara nyingi Wenger huwa ana matarajio makubwa. Ameweza kuwabakisha wachezaji wake muhimu wote kwa sasa na wanacheza mpira mkubwa mno. Kila mpinzani wao lazima aingiwe na ho...