Kama ni mfuatiliaji wa mapichapicha ya wasanii wetu katika mitandao ya kijamii basi naamini utakuwa unalifahamu hili la wasanii wawili wa Bongo Fleva Baraka Da Prince na mwanadada Naj kuwa katika mahusiano ya kimapenzi.Taarifa za kusikitisha zimemfikia Gossip Cop Soudy Brown baada ya kupenyezewa ubuyu na anayedai kuwa ni mdogo wa Baraka Da Prince
anayefahamika kwa jina la Rodgers kwamba wawili hao kwasasa wapo katika ugomvi mzito. Ugomvi ambao Baraka Da Prince hataki hata kuisikia harufu ya Naj.Na za chini ya kapeti alizopenyezewa Soudy Brown ni kwamba mwanadada Naj hana mapenzi hata kidogo na familia ya Baraka Da Prince, kiasi kwamba hadi kusababisha Mama wa Baraka Da Prince kuondoka nyumbani kwa Baraka Da Prince bila kuaga kutokana na mitofautiano ya yeye na mwanadada Naj.
Nimeiweka hapa chini interview nzima ambayo Soudy Brown aliifanya pindi alipopigiwa simu na mdogo waBaraka Da Prince, unaweza kuitazama.