SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 11 Oktoba 2016

T media news

Guardiola ana majivuno zaidi ya Mourinho’


Kocha wa klabu ya Zenit St Petersburg Mircea Lucescu amesema kwamba, kocha waManchester City Pep Guardiola ana maringo zaidi ya hasimu wake mkubwa kocha wa Manchester United Jose Mourinho.

Kocha huyo mwenye uoefu wa muda mrefu aliiambia Dolce Sport: “Mourinho ni mtu mzuri sana, lakini tumetofautiana kwenye masuala ya kifundi katika soka kwasababu mimi ni mwenye ninayependa timu yangu ishambulie muda wote.

“Timu zangu zote ambazo nimezifundisha zimevunja rekodi ya mabao. Mourinho anaonekana mwenye majivuno zaidi ya Guardiola lakini mtazamo huo ni tofauti kabisa, Guardiola anaringa zaidi.

“Lakini linapokuja suala la uwanjani, wote ni makocha wakubwa.”

City waliwafunga United 2-1 katika Uwanja wa Old Trafford mwezi Septemba, huku kwa sasa wakiwa kileleni mwa msimamo wa Premier League, alama tano zaidi ya mahasimu wao United.

Timu hizo mbili zinatarajiwa kukutana tena kwenye mchezo wa raundi ya nne ya Kombe la EFL Oktoba 26.