Cesc Fabregas amekuwa ni mtu wa benchi tangu msimu mpya wa ligi uanze chini ya meneja mpya wa Chelsea Antonio Conte.
Mpaka sasa Chelsea imeshcheza michezo mitano, lakini Cesc hajaanza katika mchezo wowote kati yote hiyo, na katika mchezo muhimu dhidi ya Liverpool walipoteza kwa mabao 2-1 Stamford Bridge Fabregas aliingia dakika za majeruhi na kuonesha kiwango kikbwa sana.
Kabla ya mchezo huo wa Ijumaa, alikuwa amecheza jumla ya dakika 26 na kuongeza zingine sita na sasa amefikisha jumla ya dakika 32.
Kwa aina ya mchezaji kama Fabregas ambaye alikuwa sehemu muhimu kwenye kikosi kilichotwaa ubingwa wa EPL msimu wa 2014/15, hali hii lazima imuwie vigumu sana.
Lakini bado anaonesha kuwa na moyo wa dhati wa kuendelea kutoa mchango wake klabuni hapo licha ya changamoto anazokutana nazo kwa sasa.
Amekuwa akifanya vyema pindi tu anapoingia uwanjani mfano mzuri ukiwa ni kwenye mchezo dhidi ya Watford wakati alipotoa pasi safi ya goli la ushindi wakati Chelsea ikiwa kwenye wakati mgumu.
Kupitia akaunti yake ya Twitter, Fabregas aliandika hivi: “It hurts a lot to be dropping points again but we must stand up strong and learn from our mistakes.
+Thank you so much for the love.
Akimaanisha: “Inauma sana kukosa pointi kwa mara nyingine tena lakini tunapaswa kusimama imara na kurekebisha makosa yetu.”
✔@cesc4official
It hurts a lot to be dropping points again but we must stand up strong and learn from our mistakes.
+Thank you so much for the love.