Ndoa ni nzuri lakini pia huwa na changamoto. Tunajua wanaume huwa hawaji tu, lakini ikiwa mwanamume ana sifa zifuatazo, basi ni mwanamume mzuri wa kukuoa
Anawasiliana nawe mara kwa mara– mwanamume anayeelewa umuhimu wa mawasiliano ni mtu mzuri wa kukuoa. Mwanamume anayekusikiliza na kukuelewa, anajua wakati wa kuongea na wa kunyamaza.
Anapenda kukaa nawe– anapenda kuwa karibu nawe na huburudika kukaa nawe bila kulazimishwa.
Anakufanya kutabasamu au kucheka– Anajua vyema nyakati za kuwa mtundu ili kukufanya kucheka au kufurahia. Huwa anapenda kukutania na lengo lake kuu huwa kukuona ukifurahi.
Tabasamu lako humfanya mwenye furaha kubwa zaidi ulimweguni.
Anakusaidia– Anasimama nawe katika hali zote, mbaya na nzuri na kukusaidia katika mambo yote. Anaamini uwezo wako zaidi ya mtu mwingine yeyote.
Anajitolea kukufunza mambo yote anayofahamu– Mwanamume ambaye hajioni kufahamu mambo yote na aliye tayari kukushirikisha katika maarifa yake ni mtu bora wa kukuoa.
Mwanamume anayetambua makosa yake-Anaelewa kuwa yeye ni binadamu na ana uwezo wa kufanya makosa. Anakubali makosa hayo na kuyarekebisha jinsi awezavyo.
Anakulinda na kukujali– Huwa anahakikisha kuwa uko salama na anapiga simu kuhakikisha kuwa uko katika hali nzuri mahali ulipo, anafanya chochote awezacho kukulinda.
Anakuelewa- Anakuelewa zaidi ya mtu mwingine yeyote, anajua mambo ambayo hukukasirisha na mambo ambayo hukufurahisha, anajua sifa zako na kuelewa vyema lengo lako maishani
Mwanamume anayekuona kama mnayetoshana -Anaamini uwezo wako na talanta, na hajioni kuwa bora kukuliko. Anaamini una sifa nzuri zisizoweza kupatikana kwa mwanamke mwingine. Anaamini unaweza kufanya mambo makubwa maishani na anakufanya kuelewa hivyo. Zaidi, huwa hana hofu ya kukutambulisha kwa marafiki wake kama ‘mwanamke wake’.Kama mwanamume hana sifa hizo, basi jua kuwa mnapotezeana wakati tu.