MAKUBWA! Licha ya hivi karibuni staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford kufunga ndoa na mfanyabiashara maarufu Bongo, Rashid Said ‘Chid Mapenzi’, aliyekuwa mpenzi wa mwanadada huyo Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameibuka na kusema bado penzi lake na mrembo huyo litaendelea kama kawa, Risasi Mchanganyiko linakuwa la kwanza kukudondoshea.
ALIANZA KWA KUKACHA HARUSI Katika harusi ya Shamsa iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita msanii huyo hakuhudhuria kabisa jambo ambalo lilisababisha gumzo kwa baadhi ya waalikwa wakiwemo wasanii wakidai kwamba ameogopa na kuona aibu kwani alishindwa kufikia hatua hiyo ya ndoa hivyo angeweza kupandwa na hasira na kufanya fujo. “Unajua nimekuja kwenye hii harusi ili nimuone tu Nay wa Mitego atakuwa katika sura ya aina gani maana huyu Shamsa alikuwa mpenzi wake na hakuweza kufikia hatua ya ndoa wakati mwanamama huyu ni wife material na anajitambua. “Lakini nimemtafuta simuoni kabisa inawezekana ameona aibu au ameepusha shari kwani yule alivyo na hasira angeweza kufanya fujo hapa,” alisikika msanii mmoja akijadiliana na mwenzake.
NAY ASAKWA Baada ya kutoonekana kwenye harusi hiyo na watu kuzua gumzo, gazeti hili lilimtafuta Nay wa Mitego ambaye alieleza kwamba hakuhudhuria sherehe hiyo kwa sababu hakualikwa pia hakuwepo Dar kabla ya kufunguka kilichopo mayoni mwake. “Shamsa hakunialika kwenye sherehe yake hivyo nisingeweza kwenda pia sikuwepo Dar nilikuwa mkoani, amefanya jambo jema kuolewa siyo mbaya,” alisema Nay wa Mitego.
AFUNGUKA MAKUBALIANO YAO Mwanahabari wetu alipozidi kumchimba Nay kuhusu penzi lake na Shamsa na maumivu atakayoyapata baada ya mrembo huyo kumilikiwa na Chid Mapenzi, mkali huyo aliyezoeleka kwa kufunguka maneno ya shombo kwa wasanii wenzake, alilisema: “Siku chache kabla ya kufunga ndoa Shamsa alinifuata na kuniambia amepata mwanaume ambaye yupo tayari kumuoa nami nikamwambia sawa aolewe maana ni jambo zuri.
PENZI PALEPALE “Kuolewa siyo tatizo na siyo kwamba ndiyo mambo mengine hayataendelea, nasema bado tunapendana sana na ndoa haizuii kitu chochote. Mambo mengine yataendelea kama kawaida.”
ALICHOANDIKA MTANDAONI Muda mchache baada ya ndoa ya Shamsa kufungwa, Nay aliandika maneno haya katika ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram; “Tangazo tangazo nasikia my cousin kaolewaaaa sasa huyo aliyemuoa ipo siku nitampiga tukio kama hiiii nina hasira.”
SHAMSA ANASEMAJE? Baada ya kusikia maneno ya Nay wa Mitego, Risasi Mchanganyiko lilimgeukia Shamsa na kumweleza ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Ninachoweza kusema ni kwamba, ninampenda sana mume wangu na ninamthamini sana, sitegemei kumsaliti wala kuachana naye mpaka Mungu atakapotutenganisha.”
WOLPER KUTOHUDHURIA Kuhusu tetesi za Jacqueline Wolper kushindwa kuhudhuria kwenye sherehe hiyo kwa kile kilichodaiwa Chid Mapenzi aliwahi kuwa mpenzi wake, Shamsa alisema; “Kiukweli sijui labda alikuwa na dharura kama ilivyokuwa kwa Wema ambaye alinipa udhuru hivyo kuhusu kuwa mpenzi wa mume wangu sijui maana namuona mume wangu ni mpya kabisa hajawahi kuwa na uhusiano na mwanamke mwingine yeyote.
” TUJIKUMBUSHE Nay na Shamsa walipamba vyombo vya habari kwa muda mfupi mwishoni mwa mwaka jana kisha wakamwagana na kuueleza umma kuwa wao watabaki kuwa marafiki wa karibu.