SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 13 Septemba 2016

T media news

Nay wa Mitego afunguka, hakuna mtu atakayenipangia muziki wa kufanya

Huenda sumu ya adhabu ya BASATA kwa Nay wa Mitego ikawa haikukolea vyema.

Ni sababu rapper huyo ameibuka na kudai kuwa, hakuna mtu anayeweza kumpangia aina ya muziki wa kufanya, na kwamba hivi karibuni ataachia wimbo uitwao ‘Utakula Jeuri Yako’ ambao ni makavu kwa kwenda mbele na huenda ukazua ‘sheshe’ jingine.

“Nobody can stop me,” alisema Nay katika mahojiano kipindi cha Extra Fleva, cha Uplands FM ya Njombe kinachoendeshwa na Ergon Elly. “Muziki wangu uko pale pale, kitu ninachowaahidi mashabiki wangu, soon, siku nikiamka tu kuna wimbo unaitwa ‘Utakula Jeuri Yako’ patawaka.”

Nay alisisitiza kuwa hata katiba hairuhusu mtu kumzuia mtu mwingine kitu cha kuongea.

Hivi karibuni Nay alifungiwa kwa ufupi kujihusisha na muziki na kupigwa faini ya shilingi milioni 1 kutokana na maudhui ya wimbo wake Pale Kati uliofungiwa.

Alisema kuwa adhabu hiyo ilikuwa na madhara kiasi kwa muziki na biashara yake.