SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 13 Septemba 2016

T media news

Maafa ya Bukoba: Kuna Usiasa au Ukosefu wa Pesa?


Kila nikijaribu kuwaza nakosa majibu ya uhakika kuhusu kilichotokea Bukoba;

Tetemeko/maafa yametokea tangu tarehe 10 September, siku ya Jumamosi, ukihesabu hadi leo Jumanne ni karibu siku ya nne sasa.

Siku zote hizi nne, viongozi wa Mkoa bado wanafanya tathimini (kwa mujibu wa repota wa PB ya clouds FM leo asbh ), serikali haijatoa msaada kwa wahanga pamoja na Muheshimiwa kuahirisha safari iliyokuwa kwenye ratiba yake. 

Kwa haraka haraka baada ya kuskia safari imekatwa nikafarijika kwamba sasa msukumo wa kuwasaidia watani zangu hawa utakuwa mkubwa lakini kila anayewatembelea huishia kuwafariji kwa mdomo tu nadhani hawa wamesahau kuwa mkono mtupu haurambwi.

Nini sababu ya ukimya huu wa serikali? Pesa hakuna au kwa sababu jimbo liko chini ya upinzani?

Kamati za maafa zinashindwa kutoa hata mahema?

Watoto, wajawazito na wazee kwa siku nne wako nje na hata chakula ni cha kubeep, hii ndo serikali ya wanyonge?

Kama tatizo ni Pesa, tokeni hadharani mpaze sauti sio wote wana moyo kama wa Kenyatta wengine hadi waombwe ndo hutoa misaada yao.

Ni mawazo yangu tu japo yamejaa huzuni.