SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 17 Septemba 2016

T media news

Jeshi la Uingereza halina uwezo wa kuilinda nchi

Image captionGeneral Sir Richard Barron

Imekuja kujulikana kuwa kamanda mmoja wa jeshi la Uingereza ameionya serikali kwamba vikosi vya jeshi la Uingereza havitoweza kuilinda nchi kukitokea shambulio kamili la kijeshi.

Jenerali Sir Richard Barrons, alieleza tathmini yake hiyo kali, kwenye barua aliyotuma kabla ya kustaafu kama kamanda (Joint Forces Command) mwezi wa Aprili.

Alisema uwezo wa jeshi umepunguzwa ili kupunguza gharama.

Image copyrightMODImage captionUwezo wa jeshi umepunguzwa ili kupunguza gharama.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema bajeti ya jeshi inaongezeka, na kwamba uamuzi uliofikiwa uliungwa mkono na wakuu wa jeshi, pamoja na Sir Richard