Alexis Sanchez amefunga mara mbili na kukosa penati na kuiongoza Arsenal kushinda mabao 4-1 dhidi ya Hull City pungufu kwenye mchezo wa Premier League uliopigwa KCOM Stadium.
Sanchez aliipa Arsenal goli la kwanza kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Alex Iwobi, lakini alishindwa kufunga bao la pili baada ya kukosa mkwaju wa penati uliosababishwa na Jake Livermore kabla ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Theo Walcott alifunga bao la pili dakika ya 55 kabla ya Robert Snodgrass kufunga bao pekee kwa Hull City kwenye mchezo huo kwa mkwaju wa penati.
Sanchez alifunga bao la tatu dakika ya 83 kabla ya Granit Xhaka kumaliza karamu ya magoli dakika ya 90 kwa Arsenal kwa kufunga bao la nne kwa shuti kali.
Dondoo muhimu
Arsenal wameshinda mechi sita kwenye Uwanja wa KCOM kwenye michuano yote, zaidi ya uwanja wowote wa ugenini mwingine.Hull City kwa mara ya kwanza wamepoteza mechi mbili mfululizo kwenye uwanja wao wa nyumbani tangu Mei 2015Sanchez amehusika kwenye magoli nane katika mechi tano alizokutana na Hull City kwenye michuano yote (magoli sita, assists mbili).Penati aliyokosa Sanchez ina maana kwamba ni mchezaji pekee wa Arsenal aliyepiga penati nyingi zaidi na kukosa zote.Arsenal hawajafungwa kwenye michezo ya ligi 26 iliyopita na timu yoyote iliyopanda daraja msimu husika (wameshinda mara 22, sare mara 4).