Mkurugenzi wa Yamoto Band na TMK Wanaume Family, Mkubwa Fella ameonekana kugonga mwamba juhudi zake za kutaka kurudisha mahusiano yake ya kazi na msanii wake wa zamani wa Kundi la TMK Family, Juma Nature.
Hapo awali Juma Nature alikuwa msanii wa Kundi la TMK Wanaume Family la Mkubwa Fella lakini baadae aliondoka na kwenda kuanzisha Kundi lake la TMK Wanaume Halisi.
Akiongea na Bongo5 Ijumaa hii, Fella amedai wasanii ambao wanamthamini ni wale ambao yupo nao.
“Mimi ndo hanitaki, anaona mimi sina maana, lakini walioona mimi na maana ndo hawa ambao nipo nao mpaka sasa,” alijibu Fella baada ya kuulizwa kama ana mpango wowote na Juma Nature kwa sasa.
Kauli hiyo inaonyesha meneja huyo ameonga mwamba juhudi zake za kutaka kumrudisha msanii huyo kundini baada ya kuhaidi mara kadhaa kufanya hivyo.