SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 16 Septemba 2016

T media news

EPL- REKODI MUHIMU ZA KUFAHAMU KUELEKEA MCHEZO WA CHELSEA NA LIVERPOOL


Ligi Kuu ya England inaendelea leo ambapo Chelsea watakuwa nyumbani Stamford Bridge kuwakaribisha Liverpool, mchezo utaofanyika saa 4:00 usiku kwa majira ya Afrika Mashariki.

Taarifa muhimu kutoka kila timu

Chelsea

David Luiz atakuwa akicheza kwa mara ya kwanza tangu arejee klabuni hapo kutoka PSG aliposajiliwa kwa ada ya paundi mil 34.

Luiz atapangwa mahsusi kuziba pengo la nahodha na beki mkongwe wa klabu hiyo John Terry, ambaye anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu aliyopata katika mchezo dhidi ya Swansea wikiendi iliyopita

Liverpool

Beki waa Liverpool Dejan Lovren anatarajiwa kurejea kikosini baada ya kukosekana kwenye mchezo dhidi ya Leicester kutokana na kusumbuliwa na macho, ambapo Liverpool walishinda mabao 4-1 win.

Philippe Coutinho atajumuishwa kikosini leo baada ya kukosa mchezo uliopita kutokana na kupumzishwa kufuatia safari ndefu kutoka Brazil.

Kauli za mameneja

Kocha wa Chelsea Antonio Conte: “David Luiz atacheza kwa mara ya kwanza na tunaamini atafanya vizuri.

“Tunataraji atacheza vizuri, na kwa umakini mkubwa. Sote tunafahamu kwamba David ni mchezaji mzuri na tunajitahidi kwa hali na mali kuhakikisha anakuwa katika hali nzuri ili kucheza katika kiwango bora.

“Nina imani naye kubwa sana. Ni mchezaji mzuri na nimeona mambo mazuri sana wakati akiwa mazoezini .”

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp juu ya Diego Costa: “Ni mpambanaji wa ukweli akiwa uwanjani. Anautumia mwili wake kisawasawa na huo ndio ubora wake. Kwenye mchezo dhidi ya Swansea alionesha ubora wa hali ya juu.

“Ni mchezaji wa kiwango cha dunia na hicho ndicho mashabiki wa soka wanaweza kuongea juu ya Costa.

“Msimu uliopita haukuwa mzuri kwa Chelsea na sasa wamerudi kwenye mstari, hivyo tunahitaji kuwa makini kwelikweli.”

Dondoo muhimu

Head-to-head

Chelsea wameifunga Liverpool mara mbili tu kwenye michezo tisa iliyopita waliyokutana kwenye dimba la Stamford Bridge (wameshinda mara 2, droo mara 3, kufungwa mara nne4).Hii ni mara ya 175 timu hizo zinakutana kwenye mechi za ushindani. Liverpool (wameshinda mara 75, Chelsea mara 61, droo mara 38).

Chelsea

Endapo watashinda mchezo wa leo, Chelsea watakuwa wamepata ushindi mara tatu mfululizo kwenye Premier League katika uwanja wao wa nyumbani kwa mara ya kwanza tangu May mwaka jana.Aston Villa ambao walishuka daraja ndio timu pekee iliyoshinda mechi chache za nyumbani kuliko Chelsea msimu uliopita.Chelsea walau wamefunga magoli mawili kwenye kila mchezo kati ya michezo minne ya ufunguzi.Diego Costa tayari amefunga mara nne – msimu uliopita ilimchukua mpaka kipindi cha Boxing Day kufikia idadi hiyo ya magoli.Antonio Conte ameshinda michezo ya ligi 21iliyopita nyumbani akiwa kama meneja, na hajafungwa kwenye michezo 30 tangu Juventus ilivyofungwa na Sampdoria Januari 2013.

Liverpool

Jumla ya idadi ya pointi 32 za Liverpool walizopata kwenye michezo 17 iliyopita inazidiwa na ile ya Manchester United tu (34).Endapo wataruhusu goli kwenye mchezo wa leo, watakuwa wamecheza michezo tisa ya ugenini bila clean sheet kwa mara ya kwanza tangu May 2005.