SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 22 Septemba 2016

T media news

Askari tisa JWTZ kizimbani kwa mauaji

ASKARI tisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ),   wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kwa mauaji ya mkazi mmoja wa Kata ya Chemchem Manispaa ya Tabora.

Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi,  Samson Kabigi, alisoma mashtaka dhidi ya watuhumiwa hao mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora,  Agatha Chigulu.

Alidai kuwa askari hao wote  wa Kikosi cha 823 Msange, walitenda kosa hilo Septemba 10, mwaka huu.

Inadaiwa kuwa askari hao waliwashambulia wananchi   mjini Tabora  baada ya mkesha wa Fiesta.

Askari hao   ni  MT 109535 Koplo Msafiri Kitwima (26) na MT 92697 Private Thobias Salum (30) wakazi wa  Kata ya Chem Chem, MT 114612 Private Shomary Hemed  (24), MT 114685 Private Yusuph Muluthary (25) na MT 114110 Private Rajab Mbasa (24).

Wengine ni MT 114142 Private Selestine Machemba (24), MT 114125 Private Said Rashid (27), MT 114118 Private Rogasian Shayo (24)  na  MT 114684 Private Yustin Mwingira (24), ambao wote ni wakazi wa Kikosi cha 823 Msange.

Mwendesha Mashtaka Kabigi, alidai washtakiwa wote kwa pamoja Septemba 10, mwaka huu saa 9.00 mchana walimuua Omary Shaban.

Washtakiwa   hawakutakiwa kujibu chochote   kwa vile  shauri lao litasikilizwa na Mahakama Kuu.  Walirudishwa makabusu  hadi Oktoba 5, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena