SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 6 Agosti 2016

T media news

Simba waipendezesha Kariakoo



Mshambuliaji mpya wa Simba, raia wa Burundi, Mavugo akizungumza na wanahabari.



Viongozi wa Klabu ya Simba wakizungumza na mashabiki Makao Makuu ya klabu hiyo
Wakiwa katika zoezi la kufanya usafi
Mashabiki wa Klabu ya Simba wakifuahia baada ya kumaliza usafi.

MAMIA ya wapenzi na mashabiki wa timu ya Simba leo asubuhi wafanya usafi katika mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya klabu hiyo ambayo kilele chake kitakuwa Jumatatu ijayo, Agosti 8 ambapo watakuwa wakisherekea miaka 80 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo.

Zoezi hilo la usafi ambalo limeifanya baadhi ya mitaa ya Kariakoo kuwa safi ukilinganisha na siku, liliongozwa Makamu wa Rais wa Simba hiyo, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ pamoja na msemaji wa klabu hiyo, Haji Marana.

Akizungumza baada ya zoezi hilo, Kaburu amewapongeza mashabiki hao kwa moyo wa kizalendo walioonyesha katika kutekeleza zoezi hilo ambalo limeifanya Kariakoo ambapo yalipo makao makuu ya klabu hiyo kuwa safi.

“Nawashuru sana lakini nawaomba pia tujitokeze kwa wingi uwanjani siku ya Jumatatu ambapo tutakuwa tukiadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwa klabu yetu ambapo pia siku hiyo ndipo tutakapowatambulisha kwenu wachezaji wetu wote tuliowasajili ambao wataiwakilisha timu yetu katika michuano ya Ligi Kuu Bara msimu ujao.”