Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika timu ya Yanga, jioni ya leo itashuka uwanjani kupambana na TP Mazembe kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi A katika michuno hiy.
mchezo huo ni wa kutafuta rekodi au kulinda heshima endapo Yanga itafanikiwa kushinda kwasababu tayari ilishatolewa kwenye mashindano lakini kwa upande wa Mazembe ni mchezo muhimu kwasababu wanatafuta nafasi ya kuongoza kundi hilo.
Yanga imeweka hadharani kikosi kitakachokabiliana na Mazembe. Yanga wanawakosa nyota wao wengi wa kikosi cha kwanza kama Cannavaro, Yondani, Bosou, Ngoma, Chirwa na wengine.
Kikosi kinachoanza:
1. Deogratius Munishi
2. Hassani Kessy
3. Mwinyi Haji
4. Andrew Vicent
5. Mbuyu Twite
6. Juma Makapu
7. Saimoni Msuva
8. Thabani Kamusoko
9. Amisi Tambwe
10. Deusi Kaseke
11. Haruna Niyonzima
Akiba: Beno Kakolanya, Oscar Joshua, Pato Ngonyani, Juma Mahadhi na Mateo Antony.
Mechi itachezwa kwenye uwanja wa Stade TP Mazembe kuanzia saa 8:30 kwa saa za DR Congo sawa na saa 9:30 kwa saa za Afrika Mashariki.