SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 6 Agosti 2016

T media news

JOYCE KIRIA AZIDI KUPINGANA NA CHADEMA ,AMUONYA MUME WAKE KUTO SHIRIKI UKUTA

HAYA NDO MANENO ALIYO ANDIKA MWANA DADA JOYCE KIRIA
Yes sikulilia ndani alipoingia matatizoni….. Niligangamala nikapaza sauti na wanangu mchana kweupeee… Haikuwa rahisi hata kidogo lakini ilinibidi kujitoa fahamu kwa ajili ya kuokoa familia yangu
Leo napoona dalili nyingine za kuingia kwenye matatizo makubwa zaidi ya haya, kamwe siwezi kukaa kimya…. Yes sintakaa kimya nimwache aende kutumbukia shimoni nitamwambia bila aibu kama nilivyompigania bila aibu .
.
Dear love, umenikasirikia sana kwa kitendo hiki ninachofanya… Lakini naomba ukumbuke wakati unapitia matatizo, ni Mimi nilikuwepo na wewe wakati wote mpz wanmtoto nililazimika kumwachisha ziwa akiwa mdogo sana akalia sana akazoea nikamwacha na Dada kila ilipokuwa tarehe ya kesi nikaja kukutia moyo mpz wangu Tabora mbali kote… Nikajikaza sanaaaa, kukuonyesha tabasamu ili kukupa Amani japo njia nzima nililia sana kwa uchungu ulilia kila uliponionamimi nilijikaza sikulia mbele yako ili nisikuache na mawazooooo….
Kila nilipokuja Gerezani kukuona uliwaulizia rafiki zako ulokuwa unawaamini sana, tena uliamini wangekuja kesho yake, hukuwaona mpaka ukatoka…ulikuwa unawaulizia kama wamenitafuta, nilikujibu hakuna aliyenitafuta mpz ukaumia sana mpz wangu… Kuna wengine hukutaka hata kuongea nao baada ya kutoka ndani na kurudi uraiani….
My love, Siko tayari kupitia mateso niliyopata love, siko tayari kukuona katika mazingira magumu kama yale mbaya zaidi ni ya KULAZIMISHA… Labda yatokee bahati mbaya… Lakini ya kwenda kuyatafuta hapana baba….. Najua tena nauhakika hauko tayari kuniona tena katika mateso kama Yale…hilo nauhakika nalo….Nimewaambia watoto wanisamehe kama nitakuwa nimekosea, lakini naimani hata wao cha moto walikiona, wasingependa baba yao aingie tena kwenye shida kama ile au zaidi ya ile
Popote ulipo jua nakupenda sana ndo maana nakulinda mume wangu kwa garama yeyote .Kwangu Mimi Familia kwanza, Taifa kwanza, chama baadae…..TAFADHALINI UKUTA WEKENI KANDO MFANYE MAZUNGUMZO MEZANI… MSIFANYE UBABE TULIZENI JAZBA KWA FAIDA YA FAMILIA ZENU NA TAIFA ZIMA….
(NYie mafala mnaosema nimwambie chumbani kwani tunakula dyudyu hapa? mxiuuuuuu zenu)