Diego Costa ameifungia tena Chelsea goli la ushindi kwa mara ya pili mfululizo wakati Chelsea walipotoka nyuma kwa bao 1 na kuibuka na ushindi wa mabao 2 dhidi ya Watford kwenye dimba la Vicarage Road.
Etienne Capoue aliwapa bao la uongozi Watford mnamo dakika ya 56 wakati huo wenyeji hao wakionekana kuutawala mchezo huo.
Lakini Michy Batshuayi ambaye aliingia kutoka benchi aliisawazishia Chelsea goli, likiwa ni goli lake la kwanza tangu atue klabuni hapo aliposajiliwa kwa ada ya paundi mil 33.
Baadaye Diego Costa alifunga bao la pili baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Cesc Fabregas na kumhadaa kipa wa Watford Heurelho Gomes huku zikiwa zimebaki dakika tatu.
Hali hii inampa kujiamini bosi mpya wa Chelsea Antonio Conte baada ya mchezo wa awali kushinda dhidi ya West Ham kwa mabao 2-1.
Dondoo muhimu
Tangu arejee kwenye ligi ya England mwaka 2014, Cesc Fabregas ana assists nyingi zaidi ya mchezaji yeyote England (26).
Hazard ametoa assist yake pili baada ya michezo 26 ya ligi.
Conte amepoteza mchezo mmoja tu kati ya 32 aliyocheza akiwa kama meneja ngazi ya klabu- ameshinda 29 na kutoka sare mara mbili.
Chelsea wamepata clean sheet moja tu kwenye michezo yao nane iliyopita ya ugenini.