Master J na Shaa wamekuwa kwenye uhusiano kwa miaka mingi sasa na wameendelea kuwa imara.
akini pamoja na kuwa hivyo, bado uhusiano wao wa kikazi una nafasi kubwa zaidi. Hali hiyo ndiyo imemfanya Shaa kujitahidi kutofautisha uhusiano wao na kazi kwakuwa kwake Master J ni bosi wake.
“Bosi wangu meaning ni CEO wa MJ Records, label iliyonisaini na ananisupport sana namshukuru mwenyezi Mungu, ni CEO lakini ni one of my best friends, nimemfamu sasa for ten years,” Shaa alikiambia kipindi cha Chill na Sky.
“He is one of my close advisors, ananishauri sana na nasikiliza sana ushauri wake, akikataa kitu nazingatia, akiniambia fanya hivi nasikiliza. Kwahiyo kama Shaa, Master ni my CEO, my boss and my very close friend, kama Sarah hayo ni ya Sarah.”
Master J na Shaa walikutana kwa mara ya kwanza kwenye mradi wa Cocacola Popstars takriban miaka 10 iliyopita.