SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 4 Aprili 2016

T media news

Wakazi wa Lubumbashi wahofia silaha nzito


Wakazi wa Lubumbashi wahofia silaha nzito
Wakazi wa eneo moja la kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamesema wana wasiwasi kuhusu uwezekano wa kuingizwa silaha nzito katika eneo hilo.
Wakazi wa mji wa Lubumbashi makao makuu ya mkoa wa Haut-katanga unaopatikana kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamesema wana wasiwasi kuhusu uwezekano wa kuingia wanajeshi pamoja na silaha nzito vikiwemo vifaru katika mji huo, katika kipindi hiki cha miezi michache iliyosalia kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.
Wakazi wa mji wa Lubumbashi wameeleza kuwa, mji huo ulianza kupokea wanajeshi tangu katikati ya mwezi Sptemba mwaka jana, siku moja baada ya wakuu wa vyama saba maarufu kwa jina la G-7 kufukuzwa katika muungano unaotawala nchini humo. Lambert Membe Omalanga msemaji wa serikali ya Kongo amesema kuwa, hatua ya serikali ya kutuma wanajeshi na silaha mpya ni jambo la kawaida. Membe ameongeza kuwa hafahamu ni kwa nini wananchi wanatiwa wasiwasi na kuwepo silaha hizo ambazo lengo lake ni kuilinda nchi.