SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 4 Aprili 2016

T media news

Ash Shabaab yamnyonga Mtanzania kwa tuhuma za ujasusi


Ash Shabaab yamnyonga Mtanzania kwa tuhuma za ujasusi
Raia wa Tanzania aliyejiunga na kundi la al Shabaab la nchini Somalia amenyongwa na kundi hilo kwa tuhuma za ujasusi.
Mtandao wa habari wa Hiiraan Online umeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, hukumu ya kifo dhidi ya Issa Jemes Mwesiga (27) raia wa Tanzania aliyejiunga na kundi la sh Shabaab mwaka 2013 ilitekelezwa na kundi hilo siku ya Jumamosi katika mji wa Jilib, katika mkoa wa Jubba Kati yapata kilomita 400 kusini mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu baada ya mahakama ya kundi hilo kumpata na hatia ya kuifanyia ujasusi Marekani.
Kwa mujibu wa mtandao huo, jaji wa mahakama hiyo alisoma hukumu hiyo mbele ya kadamnasi ya watu kabla ya kutekelezwa adhabu hiyo ya kifo katika uwanja ulio wazi.
Jaji huyo alidai kwenye hukumu yake kwamba, mtuhumiwa amekiri makosa na hivyo amehukumiwa adhabu ya kifo kwa kupigwa risasi.
Hadi tunapokea habari hii, serikali ya Tanzania haikuwa imesema chochote kuhusiana na habari hiyo.