SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 8 Aprili 2016

T media news

NGOMA: TUTAIFUNGA AL AHLY NA UBINGWA VPL NI WETU

               


                                                                                     
Image result for picha ya ngoma wa yanga



DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa Yanga Donald Ngoma amewaomba mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho wakati Yanga itakapokuwa inapata ushindi dhidi ya Al Ahly mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.


Mshambuliaji huyo aliyetua Yanga msimu huu akitokea timu ya Platinum ya Zimbabwe, alisema lengo lake ni kuona Yanga inapata ushindi mnono kesho.

Alisema anafurahi mashabiki wa Yanga wamempokea vizuri na namna ya kuwalipa ni kuwafanyia kazi itakayowapa furaha na mojawapo ni kuifunga Al Ahly kabla hawajakwenda kurudiana nchini Misri.



Image result for picha ya ngoma wa yanga
                                                                                                        

Pia amesema ndoto yake nyingine ni kuipa Yanga taji la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, jambo ambalo anaamini linawezekana. Ngoma ambaye ameshaifungia Yanga mabao 15 mpaka sasa, alisema hata mabao yake anayofunga sasa hayatakuwa na maana kama Yanga haitashinda taji la Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara msimu huu.

“Hata haya mashindano ya kimataifa tunayoshiriki sasa ni kwa sababu wenzetu walishinda ubingwa msimu uliopita, na mimi lengo langu ni kushinda taji kwenye msimu wangu wa kwanza ili tuendelee kushiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao,”alisema Ngoma.