Na Martha Magawa
Katika Kuokoa maisha ya Mtanzania anaepata matatizo yanayohitaji Upasuaji wa kichwa na mishipa ya fahamu Serikali kupitia wizara ya Afya kwa kushirikiana na Taasisi ya Mifupa MOI imefungua kozi ya upasuaji wa vichwa na mishipa ya Fahamu ili kuongeza madaktari wenye fani hiyo, kwani hadi sasa kuna madaktari nane pekee Nchi nzima.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ambapo ameainisha kuwa Tanzania ina madaktari nane pekee wanaohusika na Upasuaji wa vichwa na mishipa ya Fahamu ambapo saba kati yao wapo Hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha Upasuaji wa Mifupa (MOI) na mmoja yupo Bugando Mwanza.
“Wizara imeanzisha kozi kwa ajili ya kuongeza wataalamu wengi zaidi kwani hadi sasa tuna madaktari nane pekee ambapo saba kati yao wapo MOI na mmoja hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza”. Alisema Ummy
Waziri Ummy amewataka madaktari hao kuzunguka nchi nzima kwa ziara watakayojipangia kwa mwaka mzima waweze kuwafikia hata wasiokuwa na uwezo wa kuwafika Muhimbili na Mwanza.