SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 5 Machi 2016

T media news

Waarabu wapinga nchi za Magharibi kuingilia kati Libya

Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni yanaonyesha kuwa raia wa nchi za Kiarabu wanapinga uingiliaji kijeshi wa nchi za Magharibi huko Libya.Televisheni ya al Jazeera yenye makao yake nchini Qatar imetangaza leo utafiti mpya wa maoni ilioufanya kwa watazamaji wake kuhusu mashambulizi ya nchi za Magharibi huko Libya ambao umeonyesha kuwa, asilimia 90 ya watazamaji wa kanali hiyo ya televisheni wanapinga mashambulizi ya nchi za Magharibi dhidi ya Libya. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, raia katika nchi za Kiislamu wanapinga uingiliaji kijeshi wa nchi za Magharibi katika nchi za Kiislamu baada ya uvamiwa wa Marekani katika nchi za Afghanistan na Iraq na kudhihiri makundi ya kitakfiri na kigaidi huko Afghanistan, Syria na Iraq.Baada ya mapambano ya wananchi wa Libya yaliyoung'oa madarakani utawala wa Muammar Gaddafi, baadhi ya nchi ikiwemo Qatar, Uturuki na Saudi Arabia ziliyaunga mkono makundi ya kitakfiri na kigaidi nchini humo na kuzuia ushindi wa wananchi na kuingia madarakani serikali halali ya kidemokrasia.Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa, wanajeshi maalumu wa Ufaransa, Marekani na Uingereza waliwasili Libya siku kumi zilizopita. Nchi kama Tunisia, Algeria na Morocco ambazo ni miongoni mwa majirani wa Libya huko kaskazini mwa Afrika, siku kadhaa zilizopita pia nazo zilionya kuhusu kutumwa majeshi ya nchi ajinabi huko Libya.