SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 5 Machi 2016

T media news

Umoja wa Mataifa afichua uraia wa askari walionajisi watoto wadogo

Katika ripori yake ya kila mwaka iliyotolewa jana Ijumaa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alikri rasmi kwa mara ya kwanza kwamba askari wa kulinda amani wa umoja huo waliwabaka na kuwatumikisha vibaya katika ngono wanawake na ametoa wito wa kufanya marekebisho kwa ajili ya kuwawajibisha askari wa kulinda amani wanaotenda vitendo hivyo viovu na kuwasaidia na kuwahami wahanga wake.Shirika la Human Rights Watch (HRW) llimeripoti kuwa, miongoni mwa hatua zinazotazamiwa kuchukuliwa ni kuweka masharti magumu katika kuteua wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na kuharakisha mwenendo wa uchunguzi unaohusiana na vitendo hivyo. HRW inasema kuwa, hii ni mara ya kwaza katika historia ya Umoja wa Mataifa kwa Katibu Mkuu wake kufichua wazi uraia wa askari wa kulinda amani wanaobaka na kuwatumia vibaya wasichana na wanawake wakiwa na vazi na umoja huo, kwani awali mazungumzo ya Umoja wa Mataifa na nchi za askari wa kulinda amani wanaotenda vitendo hivyo viovu yalikuwa yakifanyika kwa siri.Sara Taylor ambaye ni mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake katika shirika la Human Rights Watch amekiri kwamba, Umoja wa Mataifa unakabiliwa na changamoto kubwa katika kuwatetea askari wake.Katika ripoti yake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa, kumeripotiwa kesi 99 za ubakaji na utumiaji vibaya wa wanawake katika masuala ya ngono. Katika mwaka 2014 kuliripotiwa kesi 80 za vitendo kama hivyo vya askari wa kimataifa. Ripoti hiyo inasema kesi 30 zimehusika na vitendo vya ubakaji au utumiaji mbaya wa wanawake katika masuala ya ngono ilivyofanywa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na kesi zilizobaki zinahusiana na askari waliotumwa kulinda amani katika nchi mbalimbali.Human Rights Watch imesema kuwa, askari wa kulinda amani kutoka nchi za Pakistan, Bangladesh, Sri Lanka, Uganda, Burundi, Jamhuri ya Congo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walihusika katika vitendo vichafu vya kunajisi wanawake na wasichana vya askari wa Umoja wa Mataifa. Vilevile baadhi ya uhalifu huo ulifanywa na askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika.Suala la uhalifu na jinai za askari wa Umoja wa Mataifa wanaolinda amani katika nchi mbalimbali limekuwa maudhui muhimu na iliyozusha mjadala mkubwa katika Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine za kimataifa za kutetea haki za binadamu. Japokuwa hapo kabla pia kuliripotiwa kesi na vitendo hivyo vya ubakaji na kuwanajisi wanawake vya askari wa kulinda amani katika nchi mbalimbali, lakini inaonekana kuwa, ongezeko la vitendo hivyo viovu limekuwa kubwa kiasi kwamba haviwezi tena kufichika na kufanywa siri.Ripoti zinaonesha kuwa, askari wengi wa kimataifa wamekuwa wakitumia fedha na chakula mkabala wa kupewa ngono au kuwanajisi watoto na wanawake, suala ambalo pia liliwahi kulalamikiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon akisema kuwa linaaibisha na kutisha.Japokuwa kumependekezwa kuwekwa masharti magumu katika uteuzi wa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa ili kuzuia vitendo viovu kama hivyo lakini inaonekana kuwa, sambamba na hatua hiyo kuna haja ya kuwepo usimamizi mkubwa zaidi kuhusu utendaji wa askari wa kimataifa wa kulinda amani na kuchukuliwa hatua na kuadhibiwa wahalifu. Awali kulifichuliwa ubakaji na vitendo vya kuwanajisi wanawake na watoto wadogo vilivyofanywa na askari wa Ufaransa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati lakini inasikitisha kuwa, hakukuchukuliwa hatua za maana dhidi ya wahalifu na faili hilo limetelekezwa.Kwa sasa askari wa Umoja wa Mataifa wanalinda amani katika nchi nyingi hususan nchi za Kiafrika zinazosumbuliwa na machafuko au vita vya ndani kama Liberia, Ivory Coast, Mali, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Sudan na Sudan Kusini. Katika nchi hizo raia wa kawaida wanasumbuliwa na ukosefu wa amani kutoka na vita vya wenyewe kwa wenyewe, na kwa msingi huo askari hao walitarajiwa kuwa kimbilio la amani na usalama kwa watu hao wanaopatwa na masaibu na si wao kuwazidishia machungu kwa kubaka wanawake na wabinti zao.Inaonekana kuwa, hatua ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ya kuweka wazi takwimu na uraia wa askari wahalifu ni tahadhari kubwa inayolazimu kufanyika mageuzi katika muundo wa taasisi hiyo ya kimataifa katika kazi ya kuteua na kuchagua wafanyakazi na askari wake wa kulinda amani katika nchi mbalimbali na kutolewa adhabu kali kwa wahusika wa vitendo viovu kama hivyo.