Watu zaidi ya Sita wanaripotiwa kuwa na ugonjwa huo na wamefikishwa katika hospitali ya mkoa wa Sumbawanga kwajili ya matibabu.
Serikali ya mji huo wa Sumbawanga imewataka wakazi wote wa mji huo kuchukuwa taadhari juu ya ugonjwa huo kwa Kunawa mikono yao kabla ya kula chakula na baada ya kula na
kufanya usafi wa mazingira.
Pia wameaswa kuwakataza watoto wao kucheza katika mitaro ambayo haitiririshi maji machafu (inayotuamisha maji) na tahadhari zinginezo kujikinga na Ugonjwa huo uliopo hivi sasa Mjini Sumbawanga