SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 11 Machi 2016

T media news

Shaa: Nipo tayari kuanza kufanya movie


Huenda siku za usoni ukamuona Malkia wa Uswazi, Shaa kwenye filamu kali ya Kitanzania.

Akiongea na Bongo5, Shaa amesema kwa muda mrefu amekuwa akishawishiwa na muongozaji wa filamu ya Homecoming, Seko Shamte aingie kwenye uigizaji wa filamu.

“Seko amenikalisha vikao viwili vitatu ananiconvince kuwa actress. Kwahiyo akiniconvince again for a movie or anything I won’t say NO,” amesema Shaa.

“Niliwahi kufuatwa hapo nyuma kufanya movie lakini nikakataa, miaka kama mitano sita iliyopita. Nahisi nilikataa kwasababu nilikuwa naona kama yaani kwa story nilizokuwa nazisikia kwamba hakuna malipo mazuri kwahiyo nikawa naona mara mia kufanya muziki kwasababu muziki unalipa vizuri, fasta kuliko movies.”

Shaa ametoka kufanya media tour kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania kupromote kazi zake hususan wimbo wake Toba uliotoka mwishoni mwa mwaka jana.