Kampuni ya Apple
Majibizano makali yameendelea kati ya serikali ya Marekani na kampuni ya Teknolojia ya Apple, baada ya kampuni hiyo kukataa kusaidia kufungua simu ya mmoja wa washambuliaji waliowauawa watu kwa kuwapiga risasi mwezi Disemba.
Idara ya sheria iliwasilisha ombi mahakamani ikisema simu ya mshambuliaji huyo huenda ina ushahidi kuhusu shambulio hilo.
Apple dhidi ya serikali ya Marekani
Pia idara hiyo imelaumu Apple kwa kuwa na ukaidi.