Makumi ya watu wameuawa baada ya kuzuka uasi wa wananchi katika mji wa Raqqa ambao kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh limeufanya mji mkuu wake ndani ya ardhi ya Syria.Uasi huo umetokea baada ya wanamgambo wapatao 200 kujitenga na kundi hilo la kigaidi na kitakfiri na kupambana na makamanda wa kundi hilo. Duru kadhaa za ndani katika mji wa Raqqa zimeripoti kuwa mapigano yamepamba moto kwa muda wa siku kadhaa baada ya kuzuka uasi miongoni mwa makamanda wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh.Duru moja imeripoti kuwa wanamgamno wapatao 200 wa kundi la Daesh ambao ni raia wa Syria wamejiunga na wakaazi wa Raqqa na kuwafanya magaidi walazimike kuweka vizuizi vya barabarani katika njia za kuingilia mjini humo.Kwa mujibu wa mashuhuda, raia wa mji wa Raqqa sasa wanavidhibiti viunga vya al-Dareiyeh, al-Ramileh, al-Ferdows, al-Ajili na al-Bakri.Baadhi ya duru zimeripoti kuwa wapiganaji wengi wanalitoroka kundi la Daesh baada ya jeshi la Syria na wapiganaji wa Kikurdi kukomboa maeneo kadhaa yanayouzunguka mji wa Raqqa pamoja na ngome kadhaa za Daesh nchini Syria.../