SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 28 Machi 2016

T media news

MESSI: NATAMANI KUCHEZA UINGEREZA NA ITALY



Na Albogast Benjamin

Nyota wa Barcelona na Argentina Lionel Messi amedai yeye ni mfuatiliaji mzuri wa ligi za EPL na Serie A na anaweza kujiunga na moja ya ligi hizo japokuwa amesisitiza anatamani kubakia Barcelona kwani anapata muda mzuri na ushirikiano kutoka kwa wachezaji wenzake.

Nahodha huyo wa Argentina muda mrefu amekuwa akihusishwa na kuhamia Uingereza kwenye klabu ya Manchester City kutokana na timu hiyo kusaini mkataba na kocha aliyemfundisha Messi kwa mafanikio makubwa Pep Guardiola.

Messi amekuwa akisisitiza kwamba yeye anataka kubaki Camp Nou, ingawa yeye alikubali kuwa hali inaweza kubadilika na yeye anaweza kulazimishwa kubadili mawazo yake.

“Mimi napenda kandanda ya Uingereza na pia soka ya Italia, natazama mechi kubwa, ” alifafanua katika mahojiano na kituo cha TV cha Misri MBC.

“Lakini kama nitakuwa tayari nitasema, nia yangu ni kukaa kwa miaka mingi ndani ya Barça na kustaafu hapa”.

“Natumaini mambo hutokea na mimi si kwamba nimebadili mawazo yangu. Katika soka huwezi kujua, na mambo yanaweza kubadilika kutoka siku moja hadi nyingine”. alisema Messi