SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 5 Machi 2016

T media news

Maafisa wa jeshi la wanamaji la Tanzania kupatiwa mafunzo Iran

Balozi wa Iran nchini Tanzania amesema maafisa wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania wamekubaliana kuendelea kufanywa kwa utaratibu maalumu safari za manowari za operesheni na za utoaji mafunzo za Iran huko nchini Tanzania.Mehdi Agha Jaafari aliyasema hayo jana katika bandari ya Dar es Salaam, kwenye hafla ya kuuaga msafara wa manowari ndogo za 39 za jeshi la wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kueleza kuwa safari ya manowari hizo imewapa izza na heshima Wairani waishio nchini Tanzania na wapenzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.Balozi wa Iran nchini Tanzania ameongeza kuwa maafisa wa kijeshi wa Tanzania wamefurahishwa na safari ya manowari za jeshi la wanamaji la Iran nchini humo na wameiomba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iisaidie nchi hiyo katika kuimarisha jeshi lake la wanamaji hususan kupitia utoaji mafunzo kwa maafisa na wanafunzi wa jeshi hilo.Admeri Mkuu wa Pili Babak Abdollahi, kamanda wa msafara wa manowari za 39 za jeshi la wanamaji la Iran amesema safari hiyo nchini Tanzania ya ukusanyaji taarifa, operesheni na utoaji mafunzo ilikuwa ya mafanikio na kuongeza kwamba kushiriki kikamilifu vikosi vya wanamaji vya jeshi la Iran katika operesheni za kuhakikisha amani na uthabiti unapatikana duniani ni ishara ya kuzidi kuongezeka nguvu na uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.Baada ya kutia nanga na kubaki kwa muda wa siku nne katika bandari ya Dar es Salaam, manowari ndogo za 39 za jeshi la wanamaji la Iran ziliondoka nchini humo jana baada ya hafla ya kuziaga iliyohudhuriwa na maafisa wa ubalozi wa Iran na wa jeshi la Tanzania.../