Kiba..
Hivi karibuni, Jokate alizungumza na wanahabari wa Global Publishers na kudai amemchoka mpenzi wake huyo hivyo ameamua kumuacha rasmi Kiba ambapo habari hiyo ilichapwa jana kwenye Gazeti la Ijumaa.
Kiba na Jokate.
“Tunamshangaa Jokate kusema eti amemchoka Kiba leo wakati anajua kitambo tu Kiba hakuwa na mpango naye. Kiba alilazimika ‘ku-fake’ penzi kwa sababu walikuwa wanafanya kazi za pamoja, hakuwa na jinsi.
Jokate..
Gazeti hili lilimtafuta Kiba katika simu yake ambapo alidai hapendi sana kuanika mambo yake binafsi kwenye vyombo vya habari lakini mmoja wa mameneja wake aliyeomba hifadhi ya jina, alifafanua suala hilo.
“Kiba hakuwa na mpango na Jokate na ndiyo maana kila siku tunapokuwa kwenye kazi zetu hapendi umtajie ishu za Jokate hata kidogo na alikuwa akisisitiza kweli lakini sisi tulikuwa tunalazimisha waendelee kwa sababu tulikuwa tunafanya kazi za pamoja,” alisema meneja huyo.