SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 22 Machi 2016

T media news

Google ilitaka kuisaidia Marekani kumpindua Rais Assad wa Syria


Google ilitaka kuisaidia Marekani kumpindua Rais Assad wa Syria
Barua pepe (email) ya mwaka 2012 iliyovuja ya Hillary Clinton inaonyesha kuwa shirika la intaneti la Google lilitoa pendekezo kwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuhusu mbinu za kuiangusha serikali ya Rais Bashar al-Assad wa Syria.
Bi. Clinton ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alipokea maelezo kuhusu mpango huo kutoka kwa Jared Cohen, mkurungezi mtendaji mwandamizi katika Google ambaye alikuwa mshauri wake hadi mwaka 2010. Cohen alisema wataalamu wa Google wangeweza kuunda aplikesheni ya umma ya kompyuta ambayo ingekuwa na ramani ya kufuatilia watu wanaomuasi Assad ili kuhimiza watu wengi zaidi waasi na wajiunge na upinzani.
Katika barua pepe hiyo, Cohen alisema kwa kuzingatia ugumu wa kupata taarifa za Syria, Google ingeshirkiana na televisheni ya Al Jazeera inayomilikiwa na ufalme wa Qatar ambao unaipinga serikali ya Assad.
Barua pepe hiyo ni sehemu ya zaidi ya Email 30,000 za Clinton ambazo zimefichuliwa na mtandao wa WikiLeaks kuhusu mawasiliano ya kieletroniki ya Clinton ambaye analaumiwa kutumia email binafsi kinyume cha taratibu wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nje.
Clinton pia aliwahi kunukuliwa akisema kuwa Marekani ndiyo iliyoanzisha mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda. Aidha hivi karibuni kulifichuka habari kuwa Hillary Clinton alisema kuanzisha vita dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni ni kwa maslahi ya utawala haramu wa Israel.
Clinton anawania uteuzi wa chama cha Democrats kugombea urais wa Marekani.