SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 22 Machi 2016

T media news

Boko Haram imeua watu 20,000 Nigeria, hasara ya $5.9bn Borno


Boko Haram imeua watu 20,000 Nigeria, hasara ya $5.9bn Borno
Benki ya Dunia imesema magaidi wa Boko Haram nchini Nigeria hadi sasa wameua watu 20 elfu na kusababisha hasara ya dola bilioni 5.9 katika jimbo la Borno.
Katika taarifa iliyochapishwa Jumanne, Banki ya Dunia imetoa tathmini yake kuhusu hujuma ya magaidi wakufurishaji wa Boko Haram kaskazini mwa Nigeria hasa katika ngome ya magaidi hao jimboni Borno kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Taarifa hiyo imesema jimbo hilo limepata hasara ya dola bilioni 5.9 kutokana na mashambulizi ya Boko Haram. Taarifa hiyo imesema kati ya hasara zilizopatikana ni hujuma za Boko Haram katika idara za serikali, vituo vya afya, shule, vituo vya polisi, nyumba na magereza. Ripoti hiyo imesema kuwa tokea Boko Haram ianzishe uasi wake Nigeria, watu elfu 20 wamepoteza maisha. Benki ya Dunia imesema imewasilisha mpango wa ujenzi mpya wa maeneo yaliyoharibiwa katika hujuma za magaidi wa Boko Haram. Aidha ripoti hiyo imesema zaidi ya watu milioni mbili wamefanywa wakimbizi kufuatia ugaidi wa Boko Haram.
Neno Boko Haram kwa ya lugha ya Kihausa lina maana ya 'elimu kutoka nchi za Magharibi ni haramu'. Kundi hilo la Boko Haram ambalo lina ufahamu usio sahihi na potovu kuhusu dini ya Kiislamu, limekuwa likitekeleza hujuma katika maeneo mbalimbali ya Nigeria hasa kaskazini mwa nchi hiyo.