SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 22 Machi 2016

T media news

Magaidi 70 wa al Shabab wauawa na jeshi la Somalia


Magaidi 70 wa al Shabab wauawa na jeshi la Somalia
Magaidi zaidi ya 70 wa kundi la kitakfiri la al Shabab wameuawa katika mapigano na Jeshi la Somalia kaskazini mwa nchi hiyo.
Afisa mwandamizi wa jeshi la Somalia amenukuliwa akisema magaidi hao 70 wa al Shaba wameuawa katika eneo lenye mamalaka ya ndani ya Puntland huku wengine 30 wakijeruhiwa. Aidha Jeshi la Somalia limeukomboa mji wa bandarini wa Garad ambao ulitekwa na magaidi wa al Shabab siku chache zilizopita.
Magaidi hao wakufurishaji wenye mfungamano na mtandao wa Al Qaeda walichukua udhibiti wa mji huo Jumatatu baada ya kuushambulia kwa kutumia idadi kubwa ya wapiganaji waliofika hapo kwa boti kadhaa. Puntland iko nje ya eneo la oparesheni za Vikosi vya Kulinda Amani vya Umoja wa Afrika Somalia AMISOM venye askari 22,000 katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
Hiyo juzi Jeshi la Kenya lilitangaza kuwaangamiza magaidi 34 wa al Shabab kufuatia mapigano makali katika maeneo mawili tafauti ya Somalia.