SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 4 Machi 2018

T media news

Serikali yatolea ufafanuzi kichwa cha treni kilichoanguka Uvinza

Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametolea ufafanuzi kuhusu kichwa cha treni kilichopata ajali siku za karibuni, kuhusishwa na vichwa vilivyokutwa bandarini vikiwa havina mwenyewe.

Waziri Mbarawa amesema kuwa kichwa hicho siyo moja ya vichwa vilivyokosa mmiliki, bali kilikuwepo mwaka mmoja kabla na kwa mujibu wa rekodi, vichwa vilivyokosa mmiliki vilianzia namba 9014 mpaka 9024.

“Kichwa kilichopata ajali ni moja ya vichwa ambavyo vilikuja mwaka mmoja uliopita hakikuwa bandarini na hivi vilivyopo sasa hivi, vilivyopo sasa vina namba kuanzia 9014 mpaka 9024 tuwe angalau tunatumia weledi kwenye kazi zetu. Picha iliyounganisha si miongoni mwa vichwa vya sasa vilivyopo bandarini nina imani teknolojia inaweza saidia maana yenyewe inatunza hebu google tu hiyo picha uangalie ni ya mwaka gani ili Kupata jawabu sahihi” alisema Mbarawa

Utata huo umeibuka baada ya kichwa kimoja cha treni kupata ajali katika eneo karibu na uvinza wakati treni hiyo ilipokuwa ikitokea Tabora kuelekea uvinza.

Soma hapa treni ya abiria yapinduka

kufuatia ajali hiyo, picha zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha kichwa cha treni chenye namba 9001 ambacho picha zake ziliwahi kusambaa hapo awali kama moja ya vichwa ambavyo havina mmiliki.

Vichwa hivyo ambavyo vilikuwa na nembo ya TRL vilikutwa bandarini na Rais Dkt John Pombe Magufuli wakati alipofanya ziara ya kushtukiza.