SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 1 Machi 2018

T media news

Rais wa Zanzibar Dkt Shein afanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amafanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mapinduzi kwa kuongeza Wizara moja zaidi, na kuwabadilishia Wizara baadhi ya Mawaziri.

Kufuatia mabadiliko hayo, shughuli za Vijana zimehamishiwa katika Wizara mpya ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo; shughli za Mazingira zimehamishiwa katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais; na shughli za Wakala wa Serikali wa Uchapaji zimehamishiwa Wizara mpya ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale.

Aidha, amewateua Naibu Mawaziri wapya wawili na kumbadilisha Wizara Naibu Waziri mmoja. Kufuatia mabadiliko hayo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hivi sasa itakuwa na Wizara 14 zenye Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:

OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZIWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi- Mheshimiwa Issa Haji Ussi GavuOFISI YA RAIS, KATIBA SHERIA, UTUMISHI WA UMMA NAUTAWALA BORAWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mheshimiwa Haroun Ali SuleimanNaibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mheshimiwa Khamis Juma MwalimOFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ – Mheshimiwa Haji Omar KheriNaibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ – Mheshimiwa Shamata Shaame KhamisOFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAISWaziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Mheshimiwa Mohamed Aboud MohamedNaibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Mheshimiwa Mihayo Juma NhungaWIZARA YA AFYAWaziri wa Afya- Mheshimiwa Hamad Rashid MohamedNaibu Waziri wa Afya – Mheshimiwa Harusi Said SuleimanWIZARA YA ARDHI, NYUMBA, MAJI NA NISHATIWaziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati – Mheshimiwa Salama Aboud TalibNaibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati – Mheshimiwa Juma Makungu JumaWIZARA YA BIASHARA NA VIWANDAWaziri wa Biashara na Viwanda – Mheshimiwa Balozi Amina Salim AliNaibu Waziri wa Biashara na Viwanda – Mheshimiwa Hassan Khamis HafidhWIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALIWaziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali – Mheshimiwa Riziki Pembe JumaNaibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amal Mheshimiwa Mmanga Mjengo MjawiriWIZARA YA FEDHA NA MIPANGOWaziri wa Fedha na Mipango – Mheshimiwa Dkt. Khalid Salum MohamedWIZARA YA HABARI, UTALII NA MAMBO YA KALEWaziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale – Mheshimiwa Mahmoud Thabit KomboNaibu Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale – Mheshimiwa Choum Kombo KhamisWIZARA YA KAZI, UWEZESHAJI, WAZEE, WANAWAKE NA WATOTOWaziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto – Mheshimiwa Maudline Cyrus CasticoNaibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto – Mheshimiwa Shadia Mohamed SuleimanWIZARA YA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVIWaziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi – Mheshimiwa Rashid Ali JumaNaibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi – Mheshimiwa Dkt. Makame Ali UssiWIZARA YA UJENZI, MAWASILIANO NA USAFIRISHAJIWaziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji – Mheshimiwa Dkt. Sira Ubwa MamboyaNaibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji – Mheshimiwa Mohamed Ahmada SalumWIZARA YA VIJANA, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZOWaziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo – Mheshimiwa Balozi Ali Abeid KarumeNaibu Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo – Mheshimiwa Lulu Msham Abdulla

Aidha, Mheshimiwa Said Soud Said na Mheshimiwa Juma Ali Khatib wanaendelea kuwa Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum.