NAFASI YA UCHAWI KWENYE KAMALI
NA. DOKTA MUNGWA KABILI…0744 000 473.
=============================================================
Watu mbalimbali wamekuwa wakitaka kujua maoni yangu kuhusu nafasi ya uchawi kwenye kamali na michezo ya bahati nasibu. Yafuatayo ndio maoni yangu.
Toka enzi na enzi watu wamekuwa wakitumia uchawi ili kupata ushindi katika kamali na katika hilo zimekuwa zikitumika kila aina ya ndumba za kichawi kuanzia wale walio tumia mashimo ya Nyegere, mafuta ya usiku, Pete za bahati, Ngekewa, Ndagu, sungura weupe nakadhalika nakadhalika.
Uchawi una nafasi kubwa sana katika kamali. Maisha ya wacheza kamali mahali popote duniani hutawaliwa na uchawi.
Uchawi huanza kutawala maisha ya mcheza kamali kuanzia siku anapo anza rasmi kucheza kamali mpaka siku atakayo ingia kaburini.
Uchawi huwatawala wacheza kamali wakiwa duniani n ahata baada ya kuondoka duniani.
Ninasema hivyo kwa sababu, moja kati ya ndumba zenye nguvu sana katika kamali ni zile zinazo tokana ama kutayarishwa kwa kutumia makaburi ya wacheza kamali mashuhuri. Wacheza kamali ninao wazungumzia hapa ni wale ambao waliyatoa na kuyatumia maisha yao yote kwenye mchezo wa kamali.
Kwa mtu ambae alitajirika kupitia Kamari, kaburi lake huwa lulu yenye thamani kubwa sana katika uchawi wa kamali . Watu hutumia kaburi hilo kutengeneza ndumba kwa ajili ya kupata mali na utajiri kwa njia ya kamali. Ndumba hizo huwasaidia kushinda kwenye kamali.
Kwa watu wengi wanapo sikia kuhusu uchawi wa makaburini, akili zao moja kwa moja huwa zinaenda kwenye uchawi wa kuzika nyota za watu, kuzika kesi, kuzika ndoa, mahusiano, biashara za watu , kuwatia watu nuksi, mabalaa na mikosi nakadhalika.
Wasicho kifahamu ni kwamba, makaburi yanaweza kutumika kutengeneza ndumba nzuri kutegemeana na nani amelala kwenye kaburi hilo.
Kwa mfano kwa wale walio fiwa na mama zao wazazi na wanataka kutengeneza ndumba za mapenzi, basi wanaweza kutengeneza uchawi mkubwa sana wa mapenzi kwa kutumia mchanga ulio chotwa kitaalamu kwenye sehemu ya moyo wa kaburi la mama ake huyo.
Sio hivyo tu, yapo makaburi ambayo mchanga wake hutumika kutengeneza ndumba ambazo ni tofauti sana na dhana iliyo jengeka miongoni mwa watu wengi kuhusu makaburi.
Kwa mfano kaburi alilala mtu aliye agwa mara mbili, kaburi alilolala mtoto wa mwaka mmoja na uchawi katika mapenzi, kaburi alilo zikwa mtu ambae msiba wake ulikaa sehemu mbili tofauti ndani ya mji mmoja , kaburi alimo lala marehemu ambae maiti yake iligombewa mahala pa kuzikwa nakadhalika.
Sasa basi mchanga kutoka kwenye kaburi alilo zikwa mtu aliye tajirika kupitia kamali hutumika kutengeneza uchawi wa kuwatajirisha watu kwa njia ya kamali.
Kinyume chake, kaburi alimo zikwa mtu ambae alifilisika kupitia kamali, mchanga wake hutumika kutengeneza uchawi wa kuwafilisi watu, kuwatia umasikini na ufukara pamoja na kuwafanya watu wenye mali nyingi kufilisika kwa kuwekeza pesa zao kwenye biashara zenye risk kubwa.
Kwa hiyo kamali ni mchezo unao husisha uchawi na ushirikina kwa kiwango kikubwa sana. Hii ni kwa sababu kamali ni mchezo wenye pesa nyingi sana. Katika ulimwengu wa kitabibu, kamali haichukuliwi tu kama mchezo wenye kuhusisha bahati ya mtu, isipokuwa huchukuliwa kama shughuli au biashara nyingine yoyote ile yenye kuleta fedha na mali nyingi kama vile biashara ya uchimbaji wa madini nakadhalika.
Kwa sababu hiyo basi wacheza kamali wakubwa wakubwa wanapo enda kwa waganga kwa ajili ya kupata ndumba za kuwawezesha kupata mafanikio kupitia kamali huwa huwa wanafanyiwa ndumba za kuleta mali na utajiri, kama ambavyo anaweza kufanyiwa mtu ambae anaingia kwenye biashara ya madini nakadhalika.
Hapa nawazungumzia wacheza kamali wanao cheza mamilioni ya mapesa kwenye makasino makubwa na ambao kamali ndio chanzo chao kikuu cha mapato.
Kamali ni mchezo wenye ushindani mkubwa sana ambao ndani yake unawahusisha watu wengi na ambao wengi wao wanatumia uchawi kushindana.
Katika ulimwengu wa kitabibu mcheza kamali huchukuliwa kama mtu anae fanya biashara nyingine yoyote yenye pesa nyingi kama vile biashara ya uchimbaji na uuzaji wa madini nakadhalika.
Na hii ndio sababu kuu wacheza kamali wanapo enda kwa waganga kwa ajili ya kupewa dawa za kuwasaidia kupata mafanikio katika kamali hupewa ndumba za mali na utajiri.
Mfano pete maalumu wanazo vaa wacheza kamali ambao watu wengi huziita pete za bahati, si pete za bahati kama watu wengi wanavyo fikiri isipokuwa ni pete maalumu za majini wa mali na utajiri. Watu wanao vaa pete hizo wanakuwa wameunganisha nyota zao na majini hao wa mali na utajiri ambao huwasaidia kuvuta na kupata mali kwa njia ya mchezo wa kamali.
Hata wale wanao chanjiwa ndumba maalumu kwa ajili ya kamali, wengi huchanjiwa ngekewa au dawa maalumu za kuvuta mali na utajiri ambao huupata kwa njia ya kamali.
Mchezo wa kamali ni mchezo ambao una miiko mingi ambayo wacheza kamali wengi huifuata na kuiishi.
Ni mchezo wenye pesa nyingi sana ambao unaweza kubadilisha maisha ya mtu usiku na mchana. Na kama wasemavyo wahenga, palipo na riziki hapakosi fitina.
Hata wewe unaetafuta riziki nautajiri kwa njia ya kamali unaweza kufanyiwa fitina pia na wachawi.
Wachawi wanajua kuwa kwenye kamali kuna mamilioni ya pesa na wanaweza kukutupia nuksi itakayo kufanya usifanikiwe kushinda kamali kwa sababu kwa wao wachawi kamali ni shughuli ama biashara nyingine yoyote ile.
Hata hivyo, kamali pia ni mchezo unao weza kumtia mtu umasikini na ufukara ndani ya muda mfupi sana.
Kwa Makala mbalimbali kuhusu ulimwengu usio onekena, tembelea: