Polisi nchini Marekani katika Jimbo la Michiganwamemkamata mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Michigan baada ya kuwapiga risasi hadi kufa wazazi wake ambao walikwenda shule anayosoma ili kumchukua kwaajili ya likizo.
Kijana huyo aliyetambulika kwa jina la James Eric Davis Jr anatuhumiwa kuwapiga risasi wazazi wake hao wakiwa katika bweni analoishi, siku moja baada ya kwenda hospitali kutokana na suala linalohusiana na matumizi wa dawa za kulevya.
Wazazi hao ni Diva Davis, 47, na James Erick Davis Sr, 48,ambao inaelezwa kuwa walipigwa risasi na mtoto wao wakiwa ghorofa ya nne ya Ukumbi wa Campbell ulioko ndani ya chuo alichokuwa anasoma ambapo ndipo bweni lake lilikuwepo.
Mwanasheria wa Jimbo la Illinois aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa familia hiyo inaishi eneo la Chicago ambapo baba wa mtoto huyo alikuwa niAskari Polisi hadi mauti ilipomfika leo.